Maria Dominika Mazzarello
Mandhari
Maria Dominika Mazzarello (Mornese, 9 Mei 1837 – Nizza Monferrato, 14 Mei 1881) alikuwa mtawa wa Piemonte, Italia Kaskazini, mwanzilishi wa Mabinti wa Bikira Maria Msaada wa Wakristo pamoja na Yohane Bosco[1].
Bikira huyo, ambaye aling’aa kwa unyenyekevu, busara na upendo, alijitolea maisha yake pamoja na shirika lake hilo kwa malezi ya Kikristo ya wasichana fukara [2].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 20 Novemba 1938, halafu mtakatifu na Papa Pius XII tarehe 24 Juni 1951.
Sikukuu yake hufanyika tarehe 14 Mei[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "MARIA DOMENICA Mazzarello, santa in "Dizionario Biografico"". Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/32600
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |